Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa mkongwe muziki Bongo, Soggy Doggy amesema kipimo cha ukubwa wa mwanamuziki ni idadi ya albamu alizonazo sokoni.
Soggy ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kwa sasa wanapaswa kulijua hilo na kutumia fursa ya kimtandao pamoja na idadi ya mashabiki wanaokutana nao katika show ili kuuza albamu.

“Bado kuna umuhimu mkubwa sana, hata duniani tu huwezi ukajiita mwanamuziki mkubwa kama albamu huna, yaani mimi nashangaa naendelea tena kushangaa Diamond alifanya show Mlimani City kiingilio elfu 50 alishindwaje kuwa na albamu ya kuwagawia wale watu waliotoa kiingilio” amesema.
Soggy Doggy ameongeza kuwa moja ya vitu anavyojivunia katika maisha yake ya muziki ni albamu, “mimi navimba nilitoa albamu tano na zilienda sokoni, juzi niliwaambia watu ni Sugu na Lady Jaydee ndio walionivuka,”.

Post a Comment

 
Top