Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Siku ya jana December 24, mtoto wa pili wa Diamond Platnumz, Prince Nillan alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandaliwa party nchini Afrika Kusini na kuhudhuriwa na wasanii wa WCB kama Harmonize, Rich Mavoko, Maromboso, Queen Darleen na wengineo, hata hivyo si wao pekee bali na member wa kundi la Mafikizolo, Nhlanhla Nciza alihudhuria.

Msanii hayo alikuwepo kwenye party hiyo kutokana na mwaliko alioupata kutoka kwa wazazi
wa Prince Nillan, Diamond na Zari. Kupitia ukurasa wake wa Instagram  Nhlanhla Nciza
ameandika;
A day well spent , Thank You fam @zarithebosslady@diamondplatnumz for inviting me to @princenillan ‘s birthday party. My son and I had such an awesome time
#PrinceNillanTurnsOne


Utakumbuka Diamond alishawahi kushirikishwa na Mafikizolo katika ngoma yao iliyokwenda kwa jina Colors of Africa, hivyo hivyo kwa upande wa Harmonize katika ngoma iitwayo Don’t Go.

Post a Comment

 
Top