Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wema Isaac Sepetu.
SIKU chache baada ya mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, kuibua hofu kwa mashabiki wake kufuatia waraka wake wa kifo alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Ijumaa limechimba na kuibua sababu tano za kutamani kufariki.


Katika waraka wake huo, Wema alieleza kuwa, kuna siku atakufa kwani hakuna atakayeishi milele.
Wema alionesha kuchoshwa na kejeli na matusi anayokutana nayo kila siku hivyo kumuomba Mungu amchukue uhai wake.

Waraka huo wa kifo wa Wema ulisomeka hivi: “Ipo siku nitakufa, hakuna anayeishi milele…Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo’ itakuwa, ‘maskini ya Mungu, dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze roho yake mahali pema…’
“Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah Wata’allah anichukue tu…Ya Dunia ni mengi sana….Kuna muda mwingine ninakufuru Mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge-exist (nisingekuwepo)… Ila acha niendelee kumtegemea yeye…

“Kila jambo hutokea kwa sababu….Hili nalo litapita… I think I need a time off social media (Nafikiri nahitaji kupumzika kwenye mitandao ya kijamii) kwa mara nyingine tena…. Siwezi jamani…”

SABABU YA KWANZA
Katika uchunguzi uliofanywa na Ijumaa, umebaini moja ya sababu zilizompelekea bidada huyo kuanika waraka huo wa kifo ni pamoja na kesi yake ya madawa ya kulevya inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.

Tangu kesi yake hiyo ya kukutwa na kutumia madawa ya kulevya ilivyoanza mwanzoni mwa mwaka huu, Wema amekuwa mtu wa nenda rudi mahakamani ambapo mpaka sasa imetajwa tena Desemba 14, mwaka huu.
Kutokana na uwepo wa kesi hiyo, mara kwa mara amekuwa akiongelewa tofauti mitandaoni jambo linalomchafulia jina na heshima yake na kitendo hicho kinaonekana kumchosha na kuamua kutoa waraka huo mzito.

SABABU YA PILI
Sababu nyingine inayoonekana wazi imempelekea kuandika waraka huo ni ishu ya kisiasa inayoendelea ya wanachama wengi kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alichopo yeye na mama yake, Mariam Sepetu na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uchunguzi umebaini kuwa, Wema na mama yake walipohamia Chadema walikuwa na imani kubwa ya kukiimarisha chama hicho, lakini kitendo cha baadhi ya wanachama kukihama chama hicho na kurejea CCM kimemkatisha tamaa na kumfanya awe njia panda na kushindwa kuamua kama abaki au aondoke.

SABABU YA TATU
Inaeleweka kuwa Wema hakuwa mtu wa kutulia na mpenzi mmoja na hiyo ilitokana na tabia za kila mwanaume anayekuwa naye katika mapenzi.
Katikati ya mwaka huu, Wema aliamua kuanzisha uhusiano na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Bakari na baadaye picha za wawili hao wakiwa kimahaba zikavuja.
Bila kujua kitu, Wema aliona amepata sehemu ya kupumzikia na kwamba kwa Bakari angeweza kumfuta machozi yote kwa sababu alikuwa na kila alichokihitaji lakini hali ikawa tofauti ambapo jamaa huyo alikuja kukamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo huko Mombasa, Kenya kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

SABABU YA NNE
Sababu nyingine iliyopeleka kuchapa waraka huo wa kifo ni kitendo cha kupishana na madili baada ya kubainika kuwa ana kesi ya madawa ya kulevya.

Ikumbukwe kuwa, Wema alitakiwa kushiriki moja kati ya tamthiliya kubwa nchini itakayoanza kuonekana hivi karibuni akiwemo na Irene Uwota na Elizabeth Michael ‘Lulu’ lakini shavu hilo likapita pembeni baada ya kubainika kuwa kesi yake ya madawa itachelewesha zoezi la kuandaa kwa kuwa atakuwa anakosa muda wa kuhudhuria lokesheni.

SABABU YA TANO
Kwa muda mrefu amekuwa akiumizwa na maneno ya watu kumsema kushindwa kupata mtoto. Amekuwa akiandamwa mara kwa mara kila anapokuwa katika uhusiano wake kiasi cha kufikia hatua ‘kufeki’ kuwa amepata mimba.
Mara nyingi amekuwa akiposti picha za watoto na kuonesha hisia zake kwa uchungu kutokupata mtoto na pia alishawahi kuweka picha akiwa na mama yake na kuandika; “Ipo siku nami nitaitwa mama.”
Licha ya kufanya vyote hivyo, amekuwa mtu wa kuandamwa kwa kukejeliwa na matusi.
Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na za nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, Dec 1, 2017. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.

Post a Comment

 
Top