Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka.
STAA wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kusikika sasa ameibuka na project mpya ya urembo ambapo ameajiri baadhi ya vijana kwa ajili ya kuendeleza urembo na kuwainua kwa ujumla.
Akiongea na Risasi Jumamosi Rose alisema kuwa kwa upande wa filamu bado yupo na anatarajia kutoa filamu mpya hivi karibuni lakini kikubwa analichokifanya ni kuwapa vijana ajira ambapo amefungua kiwanda cha urembo ‘house of beauty’ na hivi karibuni atazindua.
“Nimefanya mambo makubwa sasa baada ya ukimya wangu kwani nimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana kama kuletea taifa maendeleo na siku si nyingi nitafanya uzinduzi ambapo nitaainisha zaidi ninachokifanya,” alisema Rose Ndauka.

Stori na Na Hamida, Hassan

Post a Comment

 
Top