Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa zawadi ya kiwanja kwa kila mchezaji wa Zanzibar Heroes  na shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji.


Dkt.Shein ametoa zawadi hizo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes baada ya kufanya vizuri katika michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

“Mmeonyesha kwamba mnaweza soka katika michuano ya CECAFA, kama serikali inabidi tuwatunuku zawadi, jumla mko thelathini na tatu pamoja na wachezaji  na viongozi wa timu, kwa hiyo natoa pesa shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji na viongozi wenu pamoja na kiwanja kwa kila mchezaji na kiongozi, na viwanja vyote vitakuwa sehemu moja mtaanzisha kijiji chenu,” amesema Shein

Zanzibar Heroes walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano ya CECAFA, huku wakiwa na rekodi nzuri baada ya kumtoa bingwa mtetezi Uganda  na kuwafunga ndugu zao Kilimanjaro Stars.

Post a Comment

 
Top