Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha maombolezo katika msiba wa Joel Bendera, Sinza-Makaburini, Dar es Salaam.

RAIS Mstaafu, Jakaya Kikwete, alikuwa miongoni mwa waombolezaji wengi waliofika kutoa pole katika msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, aliyefariki jana Desemba 6 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mke wa marehemu (katikati) akiwa katika huzuni.

Msiba huo unafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza-Makaburini jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waombolezaji waliofika msibani hapo.

Akiongea msibani hapo mdogo wa marehemu, Allen Bendera, amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa Korogwe mkoani Tanga siku ya Jumapili ambapo taratibu za kumuaga jijini Dar es Salaam zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Lugalo jijini Dar na baadaye mwili kusafirishwa kuelekea mkoani Tanga.


Taswira iliivyokuwa msibani hapo.

Katika msiba huo, viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa wamefika nyumbani hapo kutoa pole.


Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas (anayezungumza)akiwa msibani hapo.
Marehemu Joel Bendela enzi za uhai wake.
Mdogo wa marehemu, Michael Bendera (kushoto) akifarijiwa.

Post a Comment

 
Top