Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Linah na Petit waliponaswa live.
AMA kweli mastaa hawaishiwi vimbwanga! Hayo yalidhihirika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita baada ya staa wa kike wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ kudaiwa kutelekeza mwanaye mchanga na kunaswa akibanjuka na jamaa ambaye ni meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Petit Man.

Tukio hilo lililonaswa na Ijumaa Wikienda lilijiri ndani ya Ukumbi wa High Sprit ulipo Jengo la IT Plaza, Posta jijini Dar kulikokuwa na pati ya usiku wa staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.
 
Wakibanjuka muziki.
Katika tukio hilo, Linah alinaswa akibanjuka na Petit Man na kuibua minong’ono kwa jinsi viguo alivyovaa vilivyokuwa vya kimitego, baadhi wageni waalikwa waliokuwa ukumbini hapo walisikika wakiteta kuwa msanii huyo muda huo alitakiwa kuwa nyumbani ili kumpa mwanaye haki ya malezi bora ya mama.
Mmoja wa wadau aliyezungumza na gazeti hili alisema kuwa, kwa jinsi Linah alivyoanza kujirusha mapema na kuvaa viguo vya kimitego ilihali mtoto akiwa bado mchanga, anaweza kuhatarisha afya ya mtoto huyo na kutengeneza mazingira ya kupata kichanga kingine kama hatakuwa makini
Wakikata viuno.
Ijumaa Wikienda lilimuwinda Linah ukumbini humo na kumuuliza kulikoni kujiachia hivyo na kwamba baadhi ya watu walikuwa wakidai alimtelekeza mwanaye mchanga ambapo alisema kuwa, hajamtelekeza mwanaye isipokuwa alimuacha sehemu salama ndiyo maana akawa na amani wakati akijiachia.
“Aaaa, usiseme nimemtelekeza bwana…unajua mwanangu ndiyo kila kitu. Unaponiona hapa ujue yuko sehemu salama ndiyo maana nina amani,” alisema Linah aliyejifungua mtoto huyo wa kike mwezi Julai, mwaka huu.

Post a Comment

 
Top