Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Aliyekuwa meneja wa Billnass amevunja ukimya baada ya kuiambia eNEWZ kuwa amejitoa kwenye lebo ya LFLG ambayo ni ndiyo iliyokuwa ikimsimamia mwanamuziki Billnass na kuanzisha lebo yake mwenyewe.

 Petit ametaja sababu kubwa ya kujitoa katika kundi hilo ni kuwa ameamua kuijitegemea na kuaanzisha  lebo yake mwenyewe inayojulikana kama "Roof Top" licha ya watu kusema kuwa yeye na Billnass wameachana kwa uhasama mkubwa. 
"Ni kweli mimi simsimamii tena Billnass lakini tuko poa na hakijaharibika chochote wala hatuna ugomvi na yeye pamoja na Mchafu. Ni mfumo wa kazi tu umebadilika na hakuna chochote kibaya na maskani pale bado ninaenda kama kawaida. Nina kampuni ambayo naimiliki mimi na mtu mwingine anayeitwa John Tojo. Kwa hiyo "Roof Top" nimeingia nao 'share',"
Hata hivyyo Petit amesema kuwa bado ataendelea kumsapati Billnass kwa kuwa walikuwa ni washkaji toka zamani kabla hata hajaanza kumsimamia.
 

Post a Comment

 
Top