Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nuh na Shilole.
ALIYEKUWA mpenzi wa msanii wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, amemfungukia mume wa Shilole aliyemuoa hivi karibuni, Ashraf Uchebe kuwa hajiamini kutokana na tabia yake ya kujistukia kwa kila posti atakayoposti mitandaoni kwa kuhisi imemlenga yeye.


Akipiga stori Over Ze Weekend, Nuh alisema alitambua kabisa Uchebe hajiamini hususani kila anapoweka ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram lazima ajibu kwa kuizodoa na kukejeli mawazo yake
Shilole na Uchebe.
“Hivi karibuni nilituma ujumbe unaomzugumzia jamaa aliyelala na bibi harusi saa chache kabla ya ndoa, baada ya posti hiyo, mshkaji kaja juu, katokwa na povu la maana, anasema atanifungia safari hadi Zenji ili kunikomesha, kimsingi ujumbe wangu ulikuwa mahususi kwa mashabiki wangu maana najiandaa na ngoma mpya, wala haikumhusu yeye. Namsihi jamaa ajiamini,” alisema Nuh.

Post a Comment

 
Top