Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Gift Stanford ‘Gigy Money’ aking’ang’aniwa na njemba.
STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ hivi karibuni alijikuta aking’ang’aniwa na njemba ambaye alidatishwa na mauno yake na kuanza kucheza naye huku akiwa amevua shati.
Chanzo kinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni, mkoani Mbeya ambako mwanadada huyo alikuwa na shoo ambayo shabiki wa kiume ‘njemba’ alipanda jukwaani huku akiwa kifua wazi na kuanza kucheza na Gigy huku akimshika kiuno vilivyo.
Alipoulizwa Gigy ilikuwaje akakubali kushikwa kiuno na njemba tena jukwaani mbele ya mpenzi wake Mo J, alisema haoni shida kwa kuwa alikuwa kazini.
“Nilikuwa nafanya shoo Mbeya shabiki ndiyo akapagawa na mauno yangu akapanda jukwaani na kuanza kucheza nami, ni kweli Mo J alikuwepo lakini alichukulia kawaida tu maana anajua ndiyo kazi yangu ilivyo,” alisema Gigy.

Post a Comment

 
Top