Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
 Msanii Nay wa Mitego amesema Godzilla na Bill Nass hawana ugomvi wowote kama inavyokuwa ikiripotiwa.
Nay wa Mitego amesema hayo mara baada ya kuwashirikisha wawili hao katika remix ya ngoma yake ‘Muda Wetu’ ambayo pia AY yumo. Akizungumza na Dj Show, Radio One Nay amesema kitu hicho kilimpa hata wepesi wa kuweza kuwakutanisha.

“Mdundo ulinifanya nimuone Godzilla, mdundo wenyewe ulinifanya nimuone Bill Nass licha kulikuwa na maneno ya huku na kule kwamba wana tofauti lakini nilikuwa nikiamini hawana tofauti” amesema Nay.
“Naweza kusema mitandano au maneno ya watu yanaweza kuchochea ugomvi ukawa mkubwa wakati ukweli watu wanakuwa hawana tofauti” ameongeza.
Ikumbukwe katika ngoma ya Nay wa Mitego ‘Moto’ alisema pengo la Gozilla katika game limefichwa na Bill Nass.

Post a Comment

 
Top