Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezindua kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo jimbo la Longido unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 na kusema kwamba wapinzani wameogopa kushiriki kwa sababu wataachwa mbali sana.

Akizindua kampeni hizo, Mwigulu amewataka wananchi wa jimbo la Longido kumchagua mgombea wa CCM, Dk. Steven Kiruswa awe mbunge wao kutekeleza ilani ya chama mapinduzi kwa kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.

Mwigulu amesema wapinzani wameogopa kuwa wataachwa mbali katika baada ya kupima uitikio wa wananchi ambao wanakubali kazi za Rais John Magufuli na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na wananchi wanaona.

Aidha amewahakikishia wananchi wajitokeze siku ya kupiga kura kwani usalama ni wa uhakika wakati wa kupiga kura.​

CHANZO NA GPL

Post a Comment

 
Top