Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
heri
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg Kheri Denice James leo amefanya ziara maalum katika kituo cha Habari cha Clouds Media Group ikiwa ni siku chache tangu alipochaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tisa Mjini Dodoma huku Ndg. Tabia Mwita akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo. 
Katika Ziara hiyo alipokelewa na Afisa Uhusiano wa CMG Ndg. Simalenga Simon na kutembelea baadhi ya Idara za chombo hicho kisha kufanya mazungumzo na baadhi ya watangazaji ikiwa ni sehemu ya kujua namna wanavyofanya kazi ya kuuhabarisha umma wa Watanzania.
Mwenyekiti huyo ambae pia kitaaluma ni Mwandishi wa Habari ametumia ziara hiyo kuwataka Vijana wote nchini kuhakikisha  Umoja, mshikamano na Upendo kwa Taifa letu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Sikukuu ya Xmass na Mwaka mpya 2018 unaendelea kudumishwa ili kutimiza ndoto aliyonayo Rais wetu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Post a Comment

 
Top