Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwanaheri Ahmed
MSANII wa Bongo Muvi, Mwanaheri Ahmed amefunguka kuwa hawezi kumwanika mpenzi wake ambaye anatoka naye kimapenzi kwa sasa, kwa sababu si sahihi kwa maadili, tamaduni na dini yake. Akizungumza na Full Shangwe, alisema kuwa kwa mila, dini na tamaduni za Kitanzania si sahihi kumuanika mwanaume wako ambaye bado hajawa rasmi, kwa sababu anakuwa ni kama mchepuko tu.


“Huwa siko tayari kuzungumzia hali yangu ya mahusiano ambayo hayana tija kimaadili, kitamaduni na hata kidini, siku Mungu akinijalia kupata mwandani wangu wa halali basi mashabiki watamjua shemeji yao,”alisema Mwanaheri.

Post a Comment

 
Top