Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nyoshi.
RAIS wa zamani wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat amempotezea mrithi wake, Patcho Mwamba kwa kusema hawezi kujibu tuhuma na kejeli zilizotolewa dhidi yake kwa kuwa anaheshimu maoni yake.

Akizungumza juu ya madai yaliyotolewa na Patcho, ya kutumia vibaya madaraka yake akiwa kiongozi, ikiwa ni pamoja na kuwanyanyasa wanamuziki wenzake, Nyoshi alisema Patcho ameongea vizuri na anaomba Mungu amsaidie ili aweze kuiongoza vizuri bendi hiyo wakati huu mwaka mpya ukitarajiwa kuanza wiki ijayo
Mwamba.
“Siwezi kujibishana na Patcho na wala siwezi kuisema vibaya FM Academia, kufanya hivyo ni kama ninajitukana mimi mwenyewe, siri ya mimi kutoka pale ninaijua na wala sijaisema sehemu yoyote, mimi nadhani ameongea vizuri kwa sababu yale ni maoni yake, hicho ndicho ninachoweza kusema,” alisema Nyoshi.

Post a Comment

 
Top