Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Muigizaji wa Bongo Muvi, Yusuf Mlela.
MUIGIZAJI wa Bongo Muvi, Yusuf Mlela amefunguka kuwa bado hajamuona mwanamke wa kumshawishi kuoa hadi pale Mungu atakapomuonesha.


Akizungumza na Za Motomoto News, Mlela alisema kuoa ni kudra za Mwenyezi Mungu, akipatikana wa kuoa ataoa ila kwa sasa bado hajampata kwa kuwa kila anayemtazama hana vigezo wala sifa.

“Kuoa ni kudra za Mwenyezi Mungu, wakati wangu ukifika na nikampata mwanamke wa kuoa itapendeza, nitaoa ila kwa sasa bado naendelea kumtafuta, nikipata mwanamke yeyote anayejua thamani ya mume na anayejiheshimu nitamuoa,” alisema Mlela.

Post a Comment

 
Top