Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa muziki Bongo, Linah amesema ni vigumu au si sawa kubadili dini kwa sababu ya mapenzi.
Linah amelazimika kusema hayo baada ya baba mtoto wake kuwa wa dini tofauti na yeye.  Muimbaji huyo ameiambia Funiko Base, Radio Five kuwa kubadili dini iwe sababu ya Mwenyenzi Mungu na si vinginevyo.

“Unajua kiimani hutakiwa kufanya vitu juu juu,  hata ukibadilisha dini ni kwa sababu ya Mungu siyo kwa sababu ya mapenzi, kwa hiyo mimi sikutaka kufanya hiyo michezo na ninaamini patalegea popote au tutaoana hivyo hivyo au Mungu mwenyewe atalegeza kwa sababu tunapendana  na tayari tuna mtoto” amesema Linah.
Pia Linah ameendelea kwa kusema ni upande upi wa familia umekuwa mgumu kuhusu jambo hilo; “kwetu nahisi ndio sana japo na kwao ni ngumu lakini kote kote kwa sababu kwao ni waislam sana na sisi ni wakristo sana”.
 

Post a Comment

 
Top