Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa Filamu Bongo, Gabo amesema wasanii wengi wa filamu nchini wanafanya kazi ambao haziwahusu.
Muigizaji huyo  amesema kitu hicho kimefanya tasnia hiyo kushuka kwa mwaka huu na kinachotakiwa sasa ni wafikirie namna ya kujifunza.

“Unapoacha kazi yako ukafanya kazi ya mwenzako ina maana unaharibu ya kwako, kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na wengi katika wao ambao walikuwa wanafanya kazi ambazo si za kwao, unajua hata ukiwa si mwanachuo ukaenda kuzindua majengo ya chuo unaweza ukawachanganya wakashindwa kufahamu wewe taaluma yako ipo wapi,” amesema Gabo.
Kauli ya Gabo inakuja mara baada ya kuonekana wasanii wengi wa Bongo Movie kujiingiza zaidi katika siasa. Utakumbuka hivi karibuni muigizaji Aunt Ezekiel alinukuliwa akisema wasanii wa movie wanaofanya hivyo kutokana wamekosa kazi za kufanya.

Post a Comment

 
Top