Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Dudubaya amefunguka na kuwachana wasanii Nuh Mziwanda, Shilole, Giggy Money na Young D na kusema ni wasanii ambao wamefanya mambo ya kijinga mwaka 2017 na kuwataka kuacha ujinga huo 2018.

Dudubaya amesema kuwa wasanii hao ndiyo wameongoza mwaka 2017 kwa kupiga mapicha ya ajabu ambayo hayana maadili yoyote kwa jamii na zimekuwa zikiwachafua wao wenyewe bila hata kujua. 
"Mfano yule Nuh Mziwanda na Shilole walipiga picha za uchi wakiwa chooni na kuzisambaza ule ni ujinga tu, mdogo wangu mimi Young D namkubali sana lakini naye alipiga picha za ajabu na Ambalulu huo nao ni ujinga, nyinyi ni wasanii mna wazaz, watoto unafikiri watoto wenu watakuwa katika mazingira gani huko mashuleni? Kwa hiyo mwaka 2017 haya mambo ya kijinga ndiyo yame 'trend' sana kuliko hata muziki wenyewe" alisema Dudubaya 
Aidha Dudubaya amewataka wasanii mbalimbali na bongo wajitahidi mwaka 2018 wasirudie makosa kama hayo tena na kuwataka wajikite katika kutengeneza muziki mzuri pia ameitaka Serikali kupitia kwa BASATA kuwashughulikia wasanii wa namna hiyo kwani wanakuwa wanaichafua tasnia ya muziki na sanaa kiujumla, hivyo ametaka wachukue hatua kali 2018.
 

Post a Comment

 
Top