Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jane Rimoy ‘Sanchi’.
Toa la moyoni! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mrembo mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ kuanika hisia zake kuwa anamzimikia vilivyo, Mbongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ na kuapa kumuondoa mazima mwanamitindo Jokate Mwegelo anayedaiwa kuendeleza uhusiano wa siri na msanii huyo.


Licha ya kuwa Kiba ana uhusiano mwingine na mrembo wa Mombasa, Kenya, inaelezwa kuwa, bado Jokate na msanii huyo anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Maumivu Per Day, wangali na uhusiano mzito wa siri na hivi karibuni walionekana pamoja katika shoo ya Fiesta, kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

TURUDI KWA SANCHI A
kizungumza na Risasi Jumamosi, Sanchi ambaye anafahamika zaidi kwa kuringishia makalio yake makubwa
mitandaoni, alisema kuwa muonekano wa Kiba na sauti yake ndivyo vitu ambavyo vimemchanganya kiasi ambacho anatamani leo au kesho aolewe naye
Mwanamitindo Jokate Mwegelo.
“Yaani Kiba ananiua muonekano wake, sauti na vitu vingine kibao natamani aniweke ndani kabisa. “Hata kama watu watanishangaa kuhusu mimi kuwa mwanamke na kusema hili lakini sitajali. “Nasema hivi kuiridhisha nafsi yangu na wala si nafsi ya mtu mwingine, kama mtu ataona nimekosea, anaweza akakaa kimya tu. “Aniache mimi na maamuzi yangu ya kusema maana kila mtu ana uhuru wa kuchagua kile anachojisikia,” alisema Sanchi.

AAPA KUMNG’OA JOKATE

Mwanamitindo huyo alienda mbele zaidi baada ya kuulizwa kuwa haogopi fujo kwani Kiba bado hajamwagana mazima na Jokate, ndipo alipoapa kufa naye. “Mimi nilikuwa najua wameshaachana lakini kama watakuwa wanaendelea basi piga ua lazima nimtoe tu maana nimekamilika pia kila idara na mimi hisia zangu zipo kwake kwa nini nijipunje?” alisema Sanchi ambaye anashikilia Taji la Figa Bomba lilotolewa hivi karibuni na Gazeti la Ijumaa.

Kama hiyo haitoshi, mwanahabari wetu alijaribu kumbana Sanchi kuhusu suala la dini kwani yeye ni Mkristo wakati Kiba ni Muislamu ambapo bila hiyana, mrembo huyo alisema yuko tayari kubadili dini bila shaka yoyote ile. “Najua Kiba ni Muislamu safi lakini ikija kwenye upande wa dini wala hakuna tabu maana waswahili wanasema kipendacho roho hula nyama mbichi, nitabadili tu hakuna namna,” alisema Sanchi.

MIKAKATI YAKE
Mrembo huyo alisema kwa kuwa kiu yake ni kuona suala hilo linatimia, atakachokifanya ni kuwa karibu na Kiba au marafiki zake ili iwe rahisi kufikisha ujumbe wake. “Najua hata kupitia gazeti anaweza kusoma na kujua kwamba nampenda lakini mimi kwa sasa nitakachokifanya nitajiweka karibu naye zaidi na ninaamini hakuna kinachoshindikana,” alisema Sanchi.

KIBA HUYU HAPA Alipotafutwa Kiba na kuelezwa hisia hizo za Sanchi, aliishia kucheka na kuuliza ni Sanchi yule maarufu kwenye mitandao na alipojibiwa ndiyo, alikata simu bila kueleza kama atamkubalia ombi lake au la. Hata alipopigiwa tena, simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa.

Post a Comment

 
Top