Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
                                        Msanii wa muziki Bongo, Nandy.
Msanii wa muziki Bongo, Faustina Charles ‘Nandy’,  amesema anaweza ku-date na Bill Nass ila siyo Dogo Janja kutokana na urafiki wao kuwa wa karibu zaidi.


Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ya ‘Kivuruge’,  ameiambia The Playlist, Times FM kuwa Bill Nass anamvutia zaidi ya Dogo Janja, hivyo anaweza kumtazama kwa jicho la pili.


“Dogo Janja ni rafiki yangu, Dogo Janja hayupo kabisa labda Bill Nass.  Watu wanavyomzungumzia naweza nikakaa mwenyewe pembeni nikasema OK,  labda nikamtazama kwa jicho la pili lakini Dogo Janja siwezi hata nikapoteza muda kumfikiria kwa sababu ni nigger wangu,” amesema Nand
Bill Nass akifanya mahojiano na Lil Ommy, mtangazaji wa kipindi cha The Playlist.
“Si kwamba (Dogo Janja) siyo type yangu, ni kijana mwenzangu lakini ni rafiki yangu ambaye najua matatizo yake na yeye anajua ya kwangu tuna-share kiasi kwamba siwezi hata kumfikiria lakini Bill naweza kumfikiria,” amesisitiza.
Katika hatua ngingine,  Nandy ameeleza kwamba licha ya kuwepo tetesi nyingi kuwa ana-date na Bill Nass hakuna jambo kama hilo na Bill Nass hajawahi hata kumueleza kuwa anamhitaji.

Post a Comment

 
Top