Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mr Poul Afunguka Alivyozalilishwa 
Msanii wa muziki wa bongo fleva Mr. Paul ambaye kwa sasa anaishi nchini Australia, amekiri kutokea kwa tukio ambalo lilimdhalilisha sana siku za nyuma mpaka kuandikwa kwenye magazeti, na kusema ni kitu ambacho hatokisahau na ilikuwa aibu kubwa kwake.
Mr. Paul amesema tukio hilo la kuandikwa kwenye magazeti kuwa amekuwa chapombe mpaka kufikia hatua ya kulala baa, lilitokana na kunywa pombe baada ya kutoka kumsindikiza mkewe alivyoondoka nchini.
"Nilikuwa nimetoka kumsindikiza mke wangu uwanja wa ndege, nikarudi nikapaki gari lioshwe, nilikuwa sijala chakula nikakutana na marafiki, tukaanza moja mbili tatu bila kula, nikasema ngoja nijiegeze kidogo kwenye viti vya baa, Kilichotokea sielewi, kwa sababu nimeamka nipo home, naona headlines kwenye magazeti jamaa kalewa analala baa sikatai ilitokea, nilikuwa ni aibu, samahani kwa mashabiki wangu, ilikuwa tukio la maramoja tu lakini sio kama cha pombe", amesema Mr. Paul.
Pamoja na hayo Mr. Paul ameomba radhi mashabiki wake kwa tukio hilo, na kusema kwamba lilitokana na stress za kummisi mkewe ambaye alisafiri.

Post a Comment

 
Top