Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari usiku wa kuamkia leo yeye na familia yake walivamiwa nyumbani kwao na kundi la wahalifu wasiojulikana wakiwa na silaha na kufyatua risasi kama mvua kwa lengo la kumshambulia Mbunge huyo.

Mbwa wa Joshua Nassari akiwa amekufa.
Hata hivyo kelele za mbwa na kutojua nyumba anayolala Nassari kati ya nyumba tatu zilizopo eneo hilo zimesaidia kumwokoa ambapo watu hao walifanikiwa kumuua mbwa wake mkubwa huku Mbunge huyo na mkewe wakifanikiwa kutoroka na kutokomea kizani usiku na baadaye kutoa taarifa Polisi.

Baadhi ya risasi zilizotumika kuua mbwa.
Kabla ya tukio hilo, Mbunge Nasari mchana wa Ijumaa alitembelea wahanga wa tukio la kushambuliwa kwa mapanga kwa baadhi ya wananchi katika kata ya Makiba siku moja kabla ya marudio ya uchaguzi mdogo wa udiwani.


U

Post a Comment

 
Top