Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Steve Nyerere na Mama Wema.
IKIWA ni takribani saa 15 tangu mwanaye ambaye ni Queen wa Filamu za Bongo na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutangaza kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), mama wa staa huyo, Mariam Sepetu amefungukia kuhusu uamuzi huo wa mwanaye na kusisitiza kwamba yeye bado ni mwanachama wa Chadema.


Mama Wema ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wanahabari nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam na kusema;
“Napenda nitamke wazi kwamba, Wema ni mtu mzima na ana maamuzi ya kwenda chama chochote atakacho, jana nimeamini kwamba Wema amehama Chadema na kwenda CCM. Safari ya siasa ni ndefu sana na ina mambo mengi.
“Napenda nitamke rasmi kwamba sina mkakati wowote wa kuhama Chadema, nitabaki kwenye mabadiliko ya upinzani kwani mabadiliko ni muhimu sana katika nchi yetu. Si vibaya yeye kwenda CCM na mwingine akaenda ACT Wazalendo na mimi kama mama nikabaki Chadema na mwingine akawa ahana chama,” alisema Mama Wema.

Akimzungumzia msanii Steve Nyerere, Mama wema alisema;
“Ukimpata mtu kama Steve Nyerere ni bomu, mimi nitaendelea kuwa Mama. Wakati Wema alipokamatwa akalazwa Kituo Kikuu cha Polisi (Sentro) -Dar, Steve hakwenda hata kumjulia hali, lakini leo anashangilia Wema kurudi CCM.
“Chadema walikuja kuniona nyumbani wakati wa matatizo, wakatujulia hali, wamemsaidia Wema mambo mengi ambayo kwa ujumla ni sawa na kunisaidia mimi. Chadema ni familia moja na mimi siwezi kuihama,” alisema Mama wema.

Post a Comment

 
Top