Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili Mke wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrina na mwenzake bado haujakamilka.

Wakili wa serikali, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi haujakamilika.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi January 8, 2018.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Miriam Mrita na Mfanyabiashara Revocatus Muyella ambapo wanakabiliwa na kesi ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017. Kwa pamoja wanadaiwa kumuuwa kwa makusudi  Dada  wa marehemu bilionea, Msuya, Aneth Msuya.
Watuhumiwa wanadaiwa kufanya tukio hilo la mauaji May 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top