Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Sanura Kasim ‘Bi Sandra’m na mumewe.
BABA wa msanii wa Bongo Fleva, Abdul Juma ‘Mzee Abdul’, amejikuta akiwaka ile mbaya baada ya kuulizwa ishu ya aliyekuwa mkewe, Sanura Kasim ‘Bi Sandra’ kuolewa na kijana aliyemzidi umri (benteni) aliyetajwa kwa jina moja la Shamte.

Bi Sandra na Shamte waliibua gumzo hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha zao zilizodaiwa kuwa ni za ndoa na kwamba wawili hao wameenda kula fungate lao pande za Afrika Kusini ‘Sauz’.
WAMBEA WAIBUA MENENO
Baada ya kuvuja kwa picha za Bi Sandra na Shamte wakiwa Sauz huku wakijinadi kuwa ni ‘kapo’ mpya mjini, wapenda ubuyu walilitafuta Ijumaa Wikienda ili kujua upande wa pili unazungumziaje hatua hiyo.
“Hata kama kila mmoja alikuwa anaishi kivyake, lakini tunafahamu udugu wao upo palepale, hebu mtafute baba wa msanii huyo mmuulize amepokeaje kitendo cha mkewe kuolewa na kijana mdogo?
“Kimsingi sisi hatujapenda. Tulitegemea angemalizia uzee wake na mzee mwenziye, mzee Abdul au hata kama si yeye, basi angalau angetafuta mtu ambaye ana umri mkubwa,” alisema mmbeya mmoja.

Wakiwa wamepozi na wajukuu zao.
MWINGINE AMUONEA HURUMA
Mmbeya mwingine aliyepiga simu chumba cha habari, alisema kuwa, anamuonea huruma Mzee Abdul kwani Shamte anatembelea nyota yake na kula maisha ambayo alipaswa kuyala yeye.
“Namuone huruma kweli Mzee Abdul, ametoka mbali na Bi Sandra, wamelala chumba kimoja pale Tandale na kule Kariakoo, leo hii mtu anaibuka from no where anakula kuku kwa mrija, inauma sana. Hili bata lilikuwa la Mzee Abdul,” alisema mnoko huyo.
IJUMAA KAZINI
Baada ya kupewa ‘tip’ hiyo na wambeya hao, Ijumaa Wikienda lilimuibukia Mzee Abdul, nyumbani kwake, Magomeni- Kagera, Dar kwa ajili ya kwenda kumsikia anazungumziaje mkewe huyo wa zamani kuolewa na benteni.
AWAKA ILEILE
Mara baada ya wanahabari kufika nyumbani kwa mzee huyo na kujitambulisha bila hata kuelezwa dhumuni, Mzee Abdul alicharuka na kusema hataki kabisa kuzungumza na wanahabari.
“Sitaki hata kuwasikia. Naomba tuheshimiane, nimesema sitaki… sitaki…sitaki kuwaona hapa nyumbani kwangu, ondokeni. Tusitake kuharibiana siku hapa,” aliwaka mkwe huyo wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
IJUMAA WIKIENDA LARUDISHA MAJESHI
Baada ya kuona mzee huyo amekuwa mbogo, wanahabari walirudi kwenda kujipanga upya na kuongeza mbinu mpya ya kuzungumza naye ili aweze kujibu kile kilichokuwa kikisubiriwa na wasomaji wake.

ATOA YA MOYONI
Baada ya kujipanga upya, wanahabari walimrudia Mzee Abdul kwa kutumia lugha ya ushawishi ili kuweza kupata wanachokitaka ambapo mzee huyo alijikuta akifunguka ya moyoni bila kupenda.
“Jamani sikilizeni, kwani mnanitafutia nini? Tatizo ni nini kwani Bi Sandra akiolewa? Hivi mlitegemea atakaa vilevile hadi lini?
“Mimi huku nina mtu wangu, tuna maisha yetu, sasa mlitegemea yeye akae mpweke hadi lini? Haya ni maisha na kila mtu anaamua kuishi anavyotaka kwa hiyo mimi sioni tatizo hata kidogo,” alisema Mzee Abdul
Mzee Abdul.
KUHUSU WIVU
Alipoulizwa kuhusu kumuonea wivu Shamte kwa kuwa anaponda raha ambazo pengine zingekuwa zake, Mzee Abdul alisema kamwe hawezi kumuonea wivu kwani kila mtu na riziki yake.
“Hiyo ni riziki yake. Kama yeye anakula raha, sawa, ndiyo riziki yake Mungu amemuandikia. Mimi nimeridhika na maisha yangu hayahaya ya kawaida,” alisema Mzee Abdul akimtakia Bi Sandra kila la heri kwenye maisha yake mapya ya uhusiano na Shamte.
TUJIKUMBUSHE
Mzee Abdul na mkewe huyo wa zamani, walikutana enzi za ujana wao na kufanikiwa kumzaa msanii wa Bongo Fleva mwaka 1989.
Mzee Abdul ambaye wakati huo alikuwa akipiga deiwaka mjini kwa kufanya dili ndogondogo zikiwemo za kuuza tiketi za majumba ya sinema, aliitunza familia yake, lakini baadaye walitengana na kila mmoja akawa anaishi kivyake.
WAKUMBUKANA

Licha ya kutengana, wakati wa uzee wao, Mzee Abdul na mkewe huyo walimaliza tofauti zao hivyo kumruhusu hata mtoto wao (msanii wa Bongo Fleva) kuwa anatoa misaada mbalimbali kwa baba yake, jambo ambalo awali lilikuwa halifanyiki

Post a Comment

 
Top