Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
SIKU ya kuzaliwa kwa msanii wa muziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alishtukizwa kwa kumwagiwa pombe na msanii mwenzake Irine Uwoya kitendo hicho kiliwashtua wakwe zake kwani ni watu walioshika dini ya kiislamu. Risasi Jumamosi baada ya kubaini hilo kutoka kwa sosi aliyekaribu na staa huyo na familia ya ukweni kwake lilimtafuta mume wa Shilole Ashrafu Uchebe ‘Uchebe’ ambaye alilifungukia suala hilo.


“Ni kweli mke wangu amemwagiwa pombe ni kwasababu alishtukizwa wazazi wamehoji na kushangazwa na hilo lakini nimewaelewesha kuwa yeye hakulitarajia alifanyiwa bila kujua, nashukuru wameelewa,” alisema Uchebe. Aidha Uchebe alisema kuwa hata hivyo anafanya kazi kubwa ya kumbadili mkewe Shilole, kwani alipomtoa ni mbali kwa vitendo na anaamini anabadilika kila siku, Mungu akijaalia atakuwa sawa na ataendana na yeye ambaye hanywi pombe.

“Mke wangu anakunywa pombe ingawa amepunguza sana kwa sasa, kwasababu ya mimi kumbadili ila bado naifanya kazi ya kumbadili siku hadi siku naamini atakaa sawa, nadhani hiyo ndio sababu ya wasanii wenzake kummwagia pombe,” alisema Uchebe.

Post a Comment

 
Top