Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mobeto.
NOVEMBA 10, mwaka huu, ilikuwa kicheko kwa upande wa mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ baada ya hasimu wake, Hamisa Hassan Mobeto kuangukia pua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Upande wa Watoto baada ya kesi yake ya madai ya matunzo ya mwanaye kwa msanii wa Bongo Fleva kutupiliwa mbali, lakini sasa mambo yamegeuka.

MOBETO AIBUKA KIDEDEA
Habari mpya ni kwamba, katika sakata hilo ambalo Mobeto alidai kutelekezwa na mwanaume huyo ambaye ni baba wa watoto wawili wa Zari, hatimaye amembwaga mwenzake huyo na kuibuka kidedea huku akisababisha kilio upande wa pili.
Ilielezwa kuwa, katika uamuzi huo uliotolewa mbele ya Hakimu Devotha Kisoka baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, ulimfurahisha Zari na timu yake (Team Zari), kiasi cha kuangusha pati ya kimyakimya wakiamini ndiyo utakuwa mwisho wa Mobeto.
SAFARI YA DUBAI
Hata hivyo, kwa mujibu wa watu wa karibu wa mastaa hao, wakati furaha ya Zari na timu yake ikipaa kwa kuamini kuwa walikuwa wameibuka kidedea, ghafla kuliibuka madai kwamba, Hamisa alionekana akila bata la hatari Dubai na mwanaume huyo, jambo lililosemekana kumfedhehesha Zari na kuizika furaha ya ushindi wa awali.
RUFAA TUPA KULE?
Ilidaiwa kuwa, ni katika kipindi hichohicho ambacho wakili wa Mobeto, Walter Goodluck alisemekana kutupilia mbali suala la kukata rufaa ya kesi hiyo, hivyo kuibua maswali kwani muda wa kufanya hivyo ulikuwa ukiyoyoma.
“Kwa taarifa yenu hakuna cha rufaa wala nini. Tayari Hamisa (Mobeto) amefanyiwa kufuru na baba mtoto wake kwa kulamba mamilioni yote aliyokuwa anadai na mpango huo utaendelea kwa utaratibu maalum aliowekeana yeye (Mobeto), wakili wake na upande wa msanii huyo.
“Unaambiwa ile safari ya Hamisa kule Dubai ilikuwa na mengi, kwanza mapenzi shatashata yalirudi kisha likaja suala la mtoto
Zari.
WAMETOKA MBALI?
“Unajua ni vigumu sana…(linatajwa jina la mwanaume aliyewazalisha Zari na Mobeto) kumchinjia Hamisa baharini maana wametoka mbali.
“Unakumbuka hata Hamisa alishawahi kusema kuwa anamjua jamaa kuliko mtu mwingine yeyote? Na akaongezea kuwa anavijua vingi kwani wamepitia kwenye mambo mengi kwa miaka tisa ya uhusiano wao?
HACHOMOKI MTU!
“Sasa hapo unadhani mbele ya Hamisa aliyejikoki vizuri kwenye mambo ya kikubwa, jamaa angechomoka? Unaambiwa sasa hivi Zari amekuwa mpole maana hizo mbwembwe za Hamisa si za nchi hii.
TEAM HAMISA VS TEAM ZARI
“Unaambiwa Team Hamisa ipo juu ile mbaya baada ya kuibwaga Team Zari ambao kwa sasa wanaonekana kabisa kuelemewa na hawana utetezi wa kueleweka hivyo inabidi wajipange sana kujibu mashambulizi.
ZARI, BABA WATOTO HAPATOSHI
“Wewe angalia hata Instagram na SnapChat, Zari na baba watoto wake hapakaliki, ni vichambo vya mafumbo mwanzo-mwisho. Inasemekana Zari ameshachukua uamuzi wa kushangaza wengi wa kummwaga kabisa baba watoto wake.
“Kuna madai kuwa Zari amekuwa akilalamika kwamba amechoshwa na jamaa yake huyo.
“Sasa hivi Zari anamkashifu waziwazi baba watoto wake juu ya tabia yake ya kuchepuka. Anaonekana amechoka na amekubali yaishe wakati Hamisa ndiyo kwanza amejitwalia umalikia,” kilitiririka chanzo chetu.
MOBETO ANACHEKA KWA DHARAAAU!
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Ijumaa lilimtafuta Mobeto ambaye alipopatikana na kuelezwa kila kitu juu ya sakata hilo, kwanza alicheka kisha akaomba aachwe kwanza ale, ashibe ndipo afunguke.
Ijumaa lilimuacha kwa muda kisha likamrudia ambapo aliulizwa juu ya ukimya katika kesi yake ya madai ya matumizi ya mtoto na ukweli juu ya taarifa kuwa ameshavuta mkwanja ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Kwanza sitaki kuzungumza sana, lakini ujue tu kuwa hakuna kesi tena na mimi nipo vizuri na baba mtoto wangu,”
Hata hivyo, Mobeto alibanwa afunguke zaidi juu ya ishu hiyo, hakuwa tayari.
TUJIKUMBUSHE
Mobeto alifikia hatua ya kumshtaki baba watoto wake huyo kwa kumdhalilisha na kutompa matunzo ya mtoto ambapo alitaka kulipwa fidia ya shilingi milioni 30 ya udhalilishaji na shilingi milioni 5 ya matumizi ya mtoto kwa kila mwezi.

Post a Comment

 
Top