Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa Bongo Flava, Ferooz amewataja wasanii watatu ambao wanatamani kufanya nao kazi kwa sasa.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Nakaza Moyo’ ameiambia XXL yaClouds Fm anatamani kufanya kazi na Aslay, Diamond na Alikiba.

“Naweza nikafanya na msanii yeyote lakini sina masuala ya utimu lakini msani kama Diamomd naweza nikafanya naye kazi, Alikiba, Aslay naye, kati ya hao watatu mmoja naweza nikafanya naye kazi na ikawa nzuri” amesema Ferooz.
Ferooz si msanii wa kwanza kusema hivyo kwani kipindi cha nyuma Country Boy alisema kitu kinachofanana na hicho kwa kueleza moja ya mipango yake ni kuja kuwakutanisha Diamond na Alikiba katika ngoma moja.
 

Post a Comment

 
Top