Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Babu Seya.
IMEBAINIKA kumbe wimbo uliowahi kutikisa katika Muziki wa Dansi wa Dunia Kigeugeu wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ni utunzi wa Babu Seya akiwa gerezani.


Hayo yamevujishwa na mpiga gitaa mahiri ambaye naye amehusika kutunga wimbo huo wa Dunia Kigeugeu na Vuta Nikuvute zilizowahi kubamba, Elombee Kichinja ambapo alisema, Babu Seya ndiye aliyemsimamia katika mafanikio yake yote ya kimuziki ikiwemo upigaji wa gitaa na utunzi wa nyimbo hizo ambazo walitunga pamoja.

“Mimi bila Mzee Nguza ukweli nisingeweza kuwa mwanamuziki unayenifahamu maana licha ya kuwa gerezani amekuwa akinifundisha mambo mbalimbali ya muziki ikiwemo kunisaidia kutunga na hata Dunia Kigeugeu ni utunzi wake pia,” alisema Elombee.

Elombee kwa sasa ameachana na Wazee wa Ngwasuma na kutimkia Bendi ya Bombadier ‘Wazee wa Kibindoke’ inayoundwa na Prezidaa wa zamani wa FM Academia, Nyoshi El Saadat.

Post a Comment

 
Top