Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
WAKULIMA wa Pamba wametakiwa kuvuna pamba yao mapema badala ya kusubiri hadi mimea yote shambani ichanue ndio waanze kuvuna kwani kufanya hivyo kusababisha ile iliyotanguliwa kuingiliwa kukomaa kupata vumbi na uchafu mwingine na hivyo kupunuza ubora.

Kauli hiyo imetolewa jana wilyani Uyui na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba wakati alikwenda kuangalia maandalizi ya kilimo cha zao hilo na kampeni za uhamasishaji wananchi kulima kwa wingi zao hilo zinazoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa kitendo cha wakulima wa pamba kusubiri mazao yote yachanua ndipo zoezi la uvunaji lianze kimekuwa kikiwasababishia kupata pamba chafu ambayo inawapelekea kupata bei ya chini.
Dkt.Tizeba aliongeza kuwa wakulima wakiona robo ya mashamba yao yako yameshachanua ni vema wakaanza kuvuna ili kulinda ubora wa pamba utakaowasaidia kuwa na pamba safi itakayowapelekea kupata bei nzuri.
“Ndugu zangu msiwe mnasubiri hadi pamba katika shamba lote ichanue ndio muanze kuvuna kwani kufanya hivyo kunasababisha iingiliwe na vumbi na takataka nyingine…jambo linalowafanya mpate bei ndogo”alisema Waziri huyo wa Kilimo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaonya wakulima wenye tabia ya kuchanganya pamba na uchafu wakati wa uuzaji wa zao hilo kuacha mara moja la sivyo wataishia jela.
Alisema akikamatwa mkulima ameweka uchafu au kumwagia maji ndani ya pamba kwa nia ya kuongeza uzito atakamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa sababu ya kuvunja Sheria inayosimamia Pamba.
“Safari hakuna mkulima atayeuza pamba chafu, wala hakuna mnunuzi atayenunua pamba chafu…nitakayemkamata akifanya hivyo nitampeleka Mahakamani ili achukuliwe hatua” alisisitiza Mwanri.
Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza zoezi la kuwakamata litawahusu pia wakulima ambao watakuwa wamechanganya pamba na mazao mengine na wanunuzi watakaochezea mizani kwa ajili ya kuwaibia wakulima.
Mwanri alisema kitendo cha uuzaji na ununuzi wa pamba chafu ndicho kilisababisha zao hilo kushuka katika kuwa la kwanza kwa uingizaji wa fedha za kigeni.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aalisema kuwa mkulima atakayelima pamba ni vema akafuata Sheria na taratibu zinazosimamia ulimaji wa zao hilo ili kuepuka kwenda jela na hivyo kutesa familia yake.

Post a Comment

 
Top