Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
IMG_0008
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika mkutano Mkuu huo uliofanyika katika hoteli ya Coconut Tree Marumbi  Mkoa wa Kusini Unguja.

IMG_0022
MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja.
IMG_0029
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano huo.
IMG_0058
MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja.
IMG_0128
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk. Ali Mohamed Shein akipiga kura ya kuwachagua viongozi wa ngazi hiyo akiwa ni miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.
IMG_0140
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipiga kura katika mkutano huo ambaye pia ni mjumbe wa mkutano.
IMG_0450 (2)
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimkabidhi taarifa ya utekelezaji ya miaka mitano ya Mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.
…………
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein 
amewataka viongozi watakaochaguliwa kupitia Mkutano Mkuu wa chama katika 
Mkoa wa Kusini Unguja, kuwa karibu na wananchi kwa kufuatilia na kushughulikia
matatizo yanayoikabili jamii.

Pia,amefafanua kuwa kila mwanachama anayepata nafasi ya uongozi ndani ya 
CCM ni lazima awe na sifa ya kufuatilia masuala mbalimbali hususan kero 
zinazowakabili wananchi ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu na 
mamlaka husika.

Rai hiyo aliitoa jana wakati akifungua Mkutano Mkuu maalum wa Uchaguzi wa CCM,
katika Mkoa huo, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Coconut Tree 
huko Marumbi Wilaya ya Kati Unguja.

Aliwambia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuwa wanatakiwa kuwachagua viongozi 
wabunifu ambao watanzisha miradi ya maendeleo itakayoongeza nguvu za kiuchumi
ndani ya Chama na kutoa ajira za kudumu kwa wananchi.

Dk.Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, 
aliwasisitiza wajumbe wa mkutano huo kutumia vizuri haki yao ya kikatiba 
kwa kuchagua viongozi imara wenye misimamo isiyoyumba katika kusimamia 
Sera za Chama na serikali kwa maslahi ya wanachi wote.

“CCM ina uzoefu mkubwa katika kufanya mageuzi ya kisera, kifikra, 
kiitikadi pamoja na kimkamkati kulingana na mabadiliko ya nyakati 
yanavyokwenda.

Aliongeza kuwa ndio maana hivi karibuni chama kimefanya mabadiliko makubwa 
katika Katiba ya Chama ili miongozo ya kikanuni iendane na mahitaji ya 
wananchi ambao ndio wapiga kura wa kuiweka CCM madarakani kwa kila uchaguzi 
mkuu.

Katika maelezo yake alisema viongozi watakaopewa dhamana ya kuongoza kwa 
kipindi cha miaka mitano wanatakiwa kutambua kuwa wao ni miongoni mwa 
wapiganaji wanaounda jeshi la CCM litakalofanikisha ushindi katika mwaka 2020.

Akitoa nasaha kwa wanachama wanaogombea na watakaoshindwa kupata nafasi za 
uongozi katika ngazi mbalimbali amewasihi wasivunjike moyo bali washirikiane 
na wenzao walioshinda na kwamba CCM ni Chama cha watu wote.

Mbali na hilo, alisema hali ya kisiasa nchini 
imeendelea kuwa na mvuto wa kipekee kwa wananchi na ushahidi wa jambo 
hilo ni ushindi uliopatikana katika uchaguzi mdogo wa madiwani Tanzania bara
ambapo CCM kimeshinda kata 42 kati ya 43.

Alisema CCM sio Chama cha mtu mmoja kama ilivyo kwa baadhi ya vyama vingine 
vya kisiasa nchini vilivyopoteza muelekeo kwa kupokonyana nafasi za uongozi.

“ Viongozi mtakaochaguliwa kemeeni makundi ya kuhatarisha uhai wa chama pamoja
 na rushwa ili kuendeleza  misingi imara ya ukombozi iliyofanywa na waasisi wa
ASP wakiongozwa na aliyekuwa Rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume aliyepigania
wanyonge wa Zanzibar kupitia mapinduzi ya mwaka 1964.”, alieleza Makamu
Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Mkoa huo,
alisifu juhudi za viongozi mbalimbali wa Chama na serikali katika kusimamia 
vizuri upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo kuimarika kwa sekta za elimu,
afya, miundombinu ya maji safi na salama pamoja na barabara.

Dk.Shein alisema kupitia mradi wa Ras Al – Khaimah unaodhamini uchimbaji wa 
visima vya maji safi na salama, Serikali ya SMZ imejidhatiti kumaliza kero 
ya ukosefu wa huduma hiyo kwa wananchi wa Mkoa huo kwa kipindi kifupi kijacho.

Alieleza kwamba utoaji wa huduma bora za kijamii na kiuchumi ndio kipimo muhimu
 cha kuipima serikali na kukitathimini Chama cha Mapinduzi kama kimetekeleza 
kwa ufanisi mambo kilichoyaahidi kwa wananchi.

“ Ni wajibu wa kila kiongozi ndani ya chama na Serikali kufanya kazi kwa 
kujituma na kwa bidii kubwa, ili wananchi wanapotutathimini na kutuhoji 
waridhike na majibu yetu kwani yatakuwa yanaendana kile tulichoahidi 
katika kampeni za uchaguzi uliopita”, alisisitiza Dk.Shein.

kwa upande wake Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan,ameeleza matarajio yake
katika uchaguzi huo ni kuchaguliwa kwa viongozi makini na watakaoivusha salama 
CCM kwa kila jambo linalotakiwa kutekelezwa kwa maslahi ya Chama.

Samia ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, alisema viongozi hao
ambao watachaguliwa wataisaidia kuondoa utendaji wa mazoea visiwani humo
na kwamba kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwenye nyanja mbalimbali.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi
alisema uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi na jumuia zake kuanzia ngazi za 
mashina hadi Mikoa umeendelea kufanyika vizuri na kwa kufuata matakwa ya 
miongozo ya kanuni za uchaguzi.

Alisema kupitia uwezo na uzoefu wa viongozi wanaochaguliwa katika Uchaguzi 
huo ni ishara ya matumaini ya Chama cha Mapinduzi kupata ushindi wa 
kihistoria katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

“Kupitia uchaguzi huu Chama kimefanya kazi ya ziada kuhakikisha viongozi wote
wanaoteuliwa kugombea nafasi za uongozi hawana sifa chafu za makundi ya 
usaliti,rushwa na kupanga safu za wagombea uongozi.” alisema Dk.Mabodi.


katika uchaguzi huo nafasi zinazogombani wa ni viongozi wa CCM Mkoa huo 
kwa nafasi za Mwenyekiti,Katibu wa Siasa na Uenezi, Wajumbe wa Halmashauri 
Kuu ya Mkoa nafasi tano(5) kutoka kusini pamoja na nafasi tano(5) kutoka kati.

Post a Comment

 
Top