Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Diamond Atoa  Ushauri Alioutoa “Ili Ufanikiwe ni Lazima Udhalilike Kwanza” 
Diamond Platnumz ameandika maneno 53 ikiwa ni saa chache baada ya Mama Watoto wake Hamisa Mobetto na Zari kufanya party Kampala Uganda kwenye sehemu mbili tofauti ndani ya usiku mmoja.
“Ili ufanikiwe ni lazma Udhalilike kwanza… yaani lazima uwaonyeshe watu kuwa kitu fulani mie nakiweza… na katika kuwaonyesha huko kuna wengine watakudharau, watakubeza na kukucheka….ila kuna wengine watakipenda, watathamini, kukikubali na kukupa nafasi”

“Maisha ndio yako hivyo… Kadri unavyozidi kuogopa na kuona “watanichukuliaje” ndio unazidi kuchelewa kufikia ndoto zako…..amka sasa ukawaonyeshe”

kutoka na caption hiyo aliyoiandika Damond Platnumz imetafsiriwa kuwa ni maneno ya kumtia moyo mzazi mwenzake Hamisa Mobetto baada ya watu kusema party ya Hamisa haijajaza watu wengi kama party ya Zari the boss lady ambazo zote zilifanyika usiku wa December 21,2017.

Post a Comment

 
Top