Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange.
CHAMA cha wananchi CUF upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kimesema kimefurahishwa na  uamuzi wa Aliyekekuwa Mbungewa  Kinondoni,  Maulid Mtulia, kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa  CUF na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM.
Akiongea,  Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF Bara, Joran Bashange, amesema wamepokea  habari hiyo kwa mshituko na pia wanampongeza kwa kuwa alikuwa upande wa Ibrahim Lipumba.
Pia amewaomba radhi wananchi wa jimbo la Kinondoni na amesema kuwa watajipanga na watawaletea mgombea mzuri zaidi ya huyo na kusema kuwa mapambano bado yanaendelea.
Sauti ya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange.

Post a Comment

 
Top