Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
BARAZA la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefanya uteuzi wa viongozi wa Baraza la Vijana la Chama hicho (BAVICHA) ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kufuatia baadhi ya viongozi wao kukihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.
 
Katika uteuzi huo, Balaza hilo limemteua aliyekuwa Katibu wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA, baada aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi kuhamia CCM. Ole Sosopo ataitumikia nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani 2018.
 
Aidha, chama hicho kimemteua ndugu Pambalu kuwa katibu wa Bavicha baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi na Ole Sosopi aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa muda.
Kabla ya maamuzi ya teuzi hizo kufanyika, Baraza la Uongozi la Chama hicho lilikutana jana na kujadiri mwenendo wa chama hicho, kuweka mikakati na malengo yao pamoja na kutoa mwelekeo mpya wa chama. Aidha chamahicho waliojadiri hali ya amani hapa nchini pamoja matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika wiki iliyopita ambapo waliambulia kata moja kati ya 43 zilizofanya uchaguzi.

Post a Comment

 
Top