Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Mwanamitindo Calisah ameshindwa kushiriki mashindano ya Mister Africa International yanayofanyika Jumamosi hii Disemba 2 huko mjini Lagos Nigeria, licha ya kutumiwa barua ya mwaliko.

Calisah ameiambia Bongo5 kwamba licha ya kuwa mashindano hayo hutakiwa washiriki kutuma maombi yao ili washiriki lakini yeye aliombwa kushiriki na kampuni ambayo inaandaa mashindano hayo.
“Haikuwa bahati yangu kwa mwaka huu kwa kuwa nimechelewa kutumiwa mwaliko, nimepokea barua November 27 wakati mashindano yamenza wiki moja nyuma na fainali ni kesho (leo),” alisema Calisah.
Aliongeza “Lakini baada ya kuwaeleza nimechelewa kupata mwaliko wao wakasema wamenitafuta toka mwezi wa 10, wakaniambia kama unaweza kuja njoo sasa lakini katika harakati za kuandaa visa siku zimeenda na kusema kweli nimepoteza nafasi kubwa sana. Hii ingenipa fursa nzuri ya kuiwakilisha nchi katika mambo ya fashion lakini mimi nadhani mwaka huu haikuwa bahati yetu ndio maana taarifa imechelewa kutufikia,”
Model huyo amesema kwa kuwa tayari ana mawasiliano kampuni hiyo basi atakuwa nao karibu zaidi ili zikitokea nafasi nyingine zimfikie mapema zaidi.
Pia alisema kwa sasa ataanza kujitanua zaidi kimataifa kwa kujitangaza kwa kuwa tayari kuna makampuni ambayo yamenza kujitokeza bila yeye kuyatafuti kitu ambayo amedai hayo ni mafanikio katika tasnia ya mitindo.
 

Post a Comment

 
Top