Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Beka Afunguka Kuhusu Kutoa Albamu" Sina Uwezo kwa Sasa" 
Msanii wa muziki Bongo, Beka Flavour amesema kwa sasa hana uwezo wa kutoa albamu kutokana na mazingira ya soko kutokuwa rafiki.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sarafina’ ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa sasa amejikita katika vitu vingine ambavyo anaona vitamuingizia fedha kwa urahisi kupitia muziki wake kuliko kuwaza kutoa albamu.


“Albamu ni kitu ambacho kipo tunakiweka pembeni kwa sababu sina uwezo wa kutoa albamu leo nikauza kwa sababu mauzo ya albamu magumu sana sasa hivi tofauti na kipindi cha nyuma ambacho wasanii walikuwa wanatengea mauzo ya albamu na inawalipa” amesema Beka.

“Kwa hiyo mimi sasa hivi natoa muziki mzuri, na target show, YouTube lakini albamu bado kwa sababu sina uwezo wa kupambana na wezi huko mtaani” ameongeza.

Licha ya kauli hiyo ya Beka kwa mwaka huu katika Bongo Flava    wasanii kadhaa wameweza kutoa albamu, miongoni mwao ni Lady Jaydee na Navy Kenzo 

Post a Comment

 
Top