Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii Baraka The Prince amedai kuwa kuna wakati ma-Dj walikuwa wanaambiwa wasicheze nyimbo zake.
Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Sometimes’ ameiambia The Base, ITV hata hivyo taarifa zilikuwa zinamfikia kutokana anaishi na watu vizuri na si kama inavyokuwa ikienezwa.

“Kuna baadhi ya Dj’s walikuwa wanaambiwa wasicheze nyimbo zangu, wengine mpaka hela wanapewa kwa ajili ya kutopiga, unakuta mpaka Dj anakufuata anakuambia unajua nimepewa mpaka hela nyimbo yako nisipige” amesema Barakah.
“Kwa hiyo hicho ni kitu cha kushukuru ingekuwa watu hawanipendi nina matatizo na watu inavyokuwa ikienezwa sidhani kama hata kuna mtu angeweza kuthubutu kunifuata na kunipa taarifa kama hizo, it means napendwa na watu na tayari nina empire yangu” ameongeza.
Hata hivyo Barakah hajaweka wazi ni kina nani hasa walikuwa wanashinikiza hivyo.

Post a Comment

 
Top