Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
ARUSHA: Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Joseph Lebulu ameng’atuka katika nafasi yake hiyo leo baada ya Baba Mtakatifu Francis kukubali ombi lililowasilishwa kwake.
Katibu mkuu wa TEC, Raymond Saba amethibitisha na kusema kuwa Papa Francis amemteua Askofu Isaac Massawe wa Jimbo Katoliki Moshi, kuwa Askofu Mkuu mpya wa Jimbo Kuu la Arusha.

Kwa mujibu wa redio Vatican, Askofu Mkuu mteule Massawe alizaliwa Juni 10, 1951 huko Mango, Jimbo Katoliki la Moshi.
Alipata upadri Juni 29,1975 na Novemba 21, 2007 aliteuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedict XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi na aliwekwa wakfu Februari 22,2008 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akisaidiana na Askofu Mkuu Lebulu na Askofu Amedeus Msarikie (sasa marehemu) wa Jimbo Katoliki la Moshi. Hivi karibuni, aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Mbulu.

Post a Comment

 
Top