Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Image result for godwin mollel
Aliyekuwa Mbunge wa Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Molel amewataka wananchi wa Siha kutoogopa akisema ametazama mbali hadi kuhama Chama hicho na kudai kuwa hawatajuta.

Akiwa kwenye Kampeni Longido Mollel amesema amehoji kama CHADEMA hawanunui watu huwa wanapeleka wapi Tsh Milioni 360 za ruzuku wanayopata kama chama kwa mwezi.
Mollel amesema kwamba "Niwaambie watu wangu wa Siha. Msiogope. Mliponichagua kuwa Mbunge nilitakiwa kulitetea taifa na kuitetea Siha. Cheo ni zaidi ya maslahi ya taifa na Siha. Msiogope nimetazama mbali na nimeona mbali hivyo hamtajuta. Natka kuwamba Rais aliyoko madarakani analitetea taifa". 
Godwin Mollel alijivua ubunge Disemba 14 mqwaka huu kwa kusema kwamba “Nimeona nia ya dhati ya Serikali CCM kutetea rasirimali za Taifa, nikaona niweze kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge ili niweze kwenda kujiunga kwa vitendo katika kulinda rasirimali za Taifa letu, aminini watu wangu wa Siha nimeona mbali katika maamuzi haya".

Post a Comment

 
Top