Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
KAMPUNI ya Uchimbaji Madini ya ACACIA imetangaza kupunguza wafanyakazi wake zaidi ya 3,000. Hatua hiyo imesababishwa na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kutokana na hali ya ukata kuikumba kampuni hiyo.
Aidha hatua hiyo imepelekea kupungua kwa shughuli za uzalishaji katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyopo wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga.

Tanzania na Barrick Gold Corporation inayomiliki migodi hiyo kwa ubia na ACACIA zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini.

Post a Comment

 
Top