Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Young Dee amesema hapendi kushindanishwa na msanii yeyote katika maisha binafsi.
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Kiutani Utani’ ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa kushindanishwa ambako ni sahihi ni katika muziki tu na si vinginevyo.

“Mashabiki kuwashindanisha wasanii ni kazi yao kama wao lakini huwa napenda sana mashabiki wanapokuwa wanashindanisha kazi kwa sababu ndio kitu kinachotukutanisha, so naamini inaleta ile chachu ya kuzidi kufanya kazi kwa bidii” amesema Young Dee.
“Lakini nje ya hapo kwenye maisha mengine nje ya kazi kabisa huwa sipendi kushindanishwa naamini kadi kufikia hapa nimepitia vitu vingi kwa hiyo historia yangu haiwezi kufanana na mtu mwingine, nikimvalisha mtu viatu vyangu hawezi akawa” amesisitiza.
Mashabiki wamekuwa wakipenda kuwashindanisha/kuwafananisha Young Dee, Dogo Janja na Young Killer.
 

Post a Comment

 
Top