Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile
akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto
linalosimamiwa na Jeshi la Polisi Tanzania.Mkurugenzi wa CDF Koshuma Mtengeti akikabidhiwa cheti cha mdau wa Dawati la Jinsia
aliyetukuka na Mhe. Naibu ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndugulile.Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile
akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Maendeleo mara baada ya kupokea vyeti kutoka Dawati
la Jinsia la Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto
linalosimamiwa na Jeshi la hilo.Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile
akiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wa Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile
akipokea Maandamano ya Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na
Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.


……………………………………………………………………..

Na Anthony Ishengoma

Takwimu za shirika la Afya Duniani zinaoenesha kuwa asilimia 35 ya wanawake ulimwenguni
ni wahanga wa vipigo na ukatili wa kingono au vyote kwa pamoja wakati hapa nchini Tanzania
taarifa ya hali ya watu na Afya ya waka 2015 inaonesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye
umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kupigwa katika kipindi cha mwaka mmoja.
Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile amesema hayo leo
jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa wa mwaka wa Dawati la Jinsia
na Watoto wa Jeshi la Polisi unaondealea kwa siku tatu.

Aidha Mhe. Ndugulile ameongeza kuwa pamoja na kuwepo ukatili wa kingono na vipigo kwa
wanawake lakini pia vitendo vya ukeketaji bado ni tatizo kubwa hapa nchini akisema liko juu
kwa kiwango cha asailimia 30 akiutaja mkoa wa Manyara kuwa na kiwango cha ukeketaji kwa
asilimia 58.
Aidha Mikoa mingine inayaoongoza kwa vitendo vya ukeketaji ni pamoja na Mkoa wa Dodoma
kwa sailimia 47,Arusha asilimia 41 ikifutiwa na Mkoa wa Mara na Singida yenye kiwango cha
asilimia 32.

Aidha ameonya kuwa ukatili wa kijinsia haukubaliki akitaja kuwa bado kuna kiwango kikubwa
cha ukatili hapa Nchini na kinagharimu Jamii na Taifa letu katika Nyanja za kijamii, kisiasa na
kiuchumi ikiwemo kuzorota kwa afya ya walengwa.
Wakati huhuo Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Kamishina wa Polisi Jamii
hapa Nchini Mussa Ally Musa amesema kuwepo na ongezeko kubwa la taarifa za ukatili wa
kijinsia na unyanyasaji kwa watoto tangu kuanzishwa kwa dawati hilo hapa Nchini ambapo kwa
kipindi cha Januari-Desemba 2016 jeshi la polisi limepokea matukio 10,551 ya ukatili wa
kijinsia kwa watoto ukilinganisha na matukio 9541 katika kipindi kama hicho 2015 na 2488 ya
mwaka 2014.

Aidha ameitaja mikoa inayoongoza kwa matukio haya kuwa ni mkoa wa Moarogoro 1403,
Rukwa 850, Singida 697,Iringa 649 na Dodoma kiwango cha matukio hayo ni 609 akiongeza
kuwa kwa upande wa Tanzania visiwani Mikoa inayoongoza ni Mkoa wa Kusini pemba, Kusini
unguja na Kasikazini unguja.
Aidha kamishina Musa ameyataja makosa ya ubakaji kuwa ndiyo yanayoongoza ambapo Jeshi la
Polisi mpaka sasa limepokea jumla ya matukio 4,423 ya ubakaji , shambulio 1,801 na shambulio
la kudhuru mwili 1,021 na matukio yan kujerui 819.

Pamoja na ongezo hilo la matukio hayo pia dawati la jinsia la jeshi la polisi limekuwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ushirikiano mdogo kutoka kwa familia husika, uchache wa
vifaa na majengo, uelewa mdogo wa wananchi na watendaji wa serikali pamija na ukosefu wa
meaneo ya kuifadhi waanga wa ukatili.

Aidha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile
ameongeza kuwa changamoto inayokabili Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ni ufinyu wa bajeti,
upungufu wa rasilimali watu, akisema serikali itaendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyoplo
huku akitaja juhudi mojawapo ni uwepo wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili
dhidi ya Wanawake na Watoto.

Post a Comment

 
Top