Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya.
MSANII wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ameagwa kwa maombi na baba mzazi wa aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana,….. na kushukuru kwa baraka hizo jambo lililovuta na kuteka hisia za watu wengi.

Katika maombi hayo mafupi, baba mzazi wa marehemu Ndikumana alimtakia safari njema Uwoya ikiwa ni pamoja na baraka tele kwake na mwanaye, Krish ambapo Uwoya aliahidi kushirikiana na familia hiyo kila atakapohitajika kwani tayari ni sehemu yao.
Baba mzazi wa aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana akimfanyia mambi Irene Uwoya. 
“Nenda na baraka zote na hakika nakupa baraka zangu zote wewe na mjukuu wangu Krish na tambua kwamba tunakupenda sana,” alisema baba mkwe wa Uwoya katika maombi hayo mafupi.
“Nawashukuru sana jamani na hakika Mungu awabariki, asante sana Burundi na Mungu awabariki,” alisema Uwoya.
Aliyoyasema kupitia akaunti yake ya Instagram
Asante baba kwa baraka zako …nashukuru mmenipokea vzuri na baraka juuu…MUNGU akubariki sanaaa…tutaonana tena nawapenda sana Mbaki salama…MUNGU ni mwema!!!asante Burundi…

Post a Comment

 
Top