Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Natamani Kufanya Kazi na Ali Kiba Katika Ujio Wangu Mpya- Sister P 
Msanii mkongwe kwenye bongo fleva, Sister P ambaye amewahi kutamba kwa ngoma kama, Anakuja,  Hey Dj na zingine amefunguka na kusema kuwa katika ujio wake mpya kwenye muziki anatamani kufanya kazi na mfalme Alikiba kwani anaamini watafanya kazi kubwa.


Sister P amesema hayo leo alipokuwa akipiga stori na mwandishi wa tovuti ya EATV na kudai kuwa akifanya kazi na Alikiba lazima itakuwa kazi kubwa na bora zaidi sababu watakuwa wamekutana wanamuziki na si wasanii.
"Kwa sasa nimejipanga vya kutosha kwa ajili ya kuanza mashambulizi mwakani mwezi wa kwanza, kuna ngoma nyingi ndani nimefanya na mtayarishaji mpya kwenye muziki anaitwa Banny Music chini ya Big Sound studio, lakini kiu yangu kubwa kufanya kazi moja na Alikiba kwani naamini itakuwa kazi kubwa zaidi sababu tutakuwa tumekutana wanamuziki na siyo wasanii" alisisitiza Sister P

Sister P ambaye hivi sasa muonekano wake umebadilika tofauti na zamani ameahidi kuwashangaza Watanzania kwa kazi zake mpya na kusema anaamini kuwa atarudi kwenye nafasi yake licha ya kukaa kimya kitambo kwenye muziki.

Post a Comment

 
Top