Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe amepata ajali katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo wilayani Kilosa mkoani hapa.

Ajali hiyo imedaiwa kutokea  saa saba usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa gari la mkuu huyo wa mkoa lilimgonga mnyama aina ya Nyati na gari hilo kuharibika vibaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa taarifa kamili ataitoa mara baada ya kukamilisha taarifa za kina za ajali hiyo.
Hata hivyo inadaiwa kwamba Mkuu huyo ndani ya gari hilo hakuwepo peke yake bali na mlinzi wake ambao wote kwa  walitoka salama.
 

Post a Comment

 
Top