Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ray C: Mwaka 2018 Utakuwa wa Recho Nafasi Yake Kwenye Muziki Bado Ipo Pale Pale 
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Ray C amemueleza msanii mwenzake Recho kuwa nafasi yake kwenye muziki bado ipo pale pale kinachotakiwa ni yeye ni kuamka na kufanya kazi.


Ray C ameeleza kuwa anaamini mwaka 2018 utakuwa wa Recho kwa sababu wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa katika Bongo Flava hawafiki hata wanne. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Ray C ameandika;

Kuna watakaokwambia hufai! Kuna watakaokwambia umefeli! Kuna watakaokukatisha tamaa na kutamka kwako waziwazi kuwa wakati wako umepita huwezi tena! Kuna watakaomua kutokukusapoti kwa sababu tu wameamua na hawaoni faida tena kwako! Nilishatamkiwa hivyo pia na nisingekuwa najitambua ningeshakata tamaa Kabisa ya kuingia Studio tena!

Lakini nikwambie nini mdogo wangu!Milima na mabonde kwenye maisha ndio inatufanya kuwa binadamu sababu aliekamili ni Mungu tu na ndio maana kuna neno linasema Nobody is perfect aliekamili ni Mungu Peke yake! Usiyumbishwe na mwanadamu na wala usifikirie hata siku moja kuwa huwezi sababu unaweza sana na umebarikiwa sauti! Sasa amka tena simama kama Recho! Maana recho ni mmoja tu hatotokea mwingine!Umeshajiwekea jina na una mashabiki wengi nikiwepo mimi dada ako! Nafurahi kukuona tena!umependeza sana!.

Naaamini unarekodi! 2018 is yours mama! Gemu bado liko waziii Kabisa nikihesabu wasanii wa kike wanaofanya vizuri sasa hawafiki hata wanne!!! !Bado nafasi yako iko palepale kama Recho!Meseji hii ni yako na yangu pia (na kwa yeyote yule anaekaribia kukata tamaa na haya Maisha) sababu uwanja ni wetu sote tena wa bure kabisa kama pumzi tulivyopewa bure) Kinachohitajika ni bidii tu ya kazi tuwafurahishe mashabiki wetu baaas! Asiyetupenda kimpango wake! I love you Tag her for Me………….

Kabla ya kupotea kimuziki Recho walikuwa akifananishwa sana na Ray C kutokana na uimbaji wake kitu kilichopelekea wengi kuamini huenda wasingekuwa na mahusiano mazuri hata hivyo hakuna jambo kama hilo kwani hata Ray C alishafanya cover ya ngoma ya Recho ‘Upepo’. 

Post a Comment

 
Top