Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo aliyepata kuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo.Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA Bw. Lawrence Masha akiomba na kukubaliwa kurudi CCM.Aliyekuwa mwanachama mwandamizi wa ACT Bi. Edna sunga akiomba kurudi na kukaribishwa CCM mbeleAliyekuwa Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akiomba na kukaribishwa kurudi CCM.
Aliyekuwa Mshauri wa Chama cha ACT Wakili Albert Msando akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Bw. Patrobas Katambi akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 201
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) ambayo inaendelea na vikao vyake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo iliwapokea na kuwarudisha katika chama hicho wanachama kadhaa kutoka vyama vya upinzani ambao walijitokeza mbele ya kujieleza na hatimaye kuomba kujiunga na chama hicho.
Miongoni mwa wanachama walipokolewa ni Profesa Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Edna Sunga (wote kutoka ACT-Wazalendo) (kutoka ACT-Wazalendo), Lawrence Masha na Patrobas Kitambi (Chadema) na wengineo.

Post a Comment

 
Top