Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga.
Nairobi, Kenya. Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga amedai atakula kiapo kama “rais wa watu” Desemba 12.Akiwahutubia wafuasi wake katika barabara ya Mayanja baada ya kutawanywa na polisi kwenye viwanja vya Jacaranda, alisema atatumia Ibara ya 1 kuapa inayosema mamlaka ya nchi yanatoka kwa watu.Mimi si mwoga. Mimi nitaapishwa Siku ya Jamhuri, mimi ndiye rais halali,” alisema akijibu malalamiko ya wafuasi wake waliosikia awali akisema hawezi kula kiapo ili asichafue taswira yake kimataifa.Awali mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Jacaranda ili kuomboleza watu waliouawa na polisi hivi karibuni ulisambaratishwa na polisi.Polisi kuanzia mapema asubuhi walifunga eneo lote la Jacaranda ambako ingefanyika misa hiyo ya kumbukumbu sambamba na tukio la Rais Uhuru Kenyatta kuapishwa kuongoza muhula wa pili wa miaka mitano baada ya kushnda uchaguzi wa marudio Oktoba 26.Magari makubwa ya polisi yalionekana yakiranda eneo hilo na watu waliojikusanya walitawanywa kwa mabomu ya machozi.
Baadaye Nasa walijikusanya barabara ya Mayanja

Post a Comment

 
Top