Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, katika kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa Bodi na baadhi ya watendaji wa Wakala huo katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam leo.

2
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Dkt. William Nshama, akizungumza na wajumbe wa Bodi na baadhi ya watendaji wa Wakala wa Majengo (TBA), katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam leo, kujadili maendeleo ya utendaji kazi wa Wakala huo.
3
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Majengo (TBA), Dkt. Edward Ngwale  akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa Bodi na baadhi ya watendaji wa Wakala huo katika ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam leo.
4
Wajumbe wa Bodi wa Wakala wa Majengo (TBA), wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam leo, kujadili maendeleo ya utendaji kazi wa Wakala huo.
5
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam leo, kujadili maendeleo ya utendaji kazi wa Wakala huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Post a Comment

 
Top